Kiswahili Dadisi – Mazoezi ya lugha Darasa la 2, Kitabu cha Mwanafunzi

R25,21

Mazoezi ya Lugha Gredi 2 Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa upekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa mpya wa Umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika. Aidha, vina mazoezi murua ambayo yatampa mwanafunzi hamu ya kujifunza. Pia vinakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masualaibuka. Katika Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi 2, utapata: • mada zilizopangwa kwa kuzingatia muainisho wa mtalaa mpya • mifano halisi ya miktadha ambapo lugha hutumika • mazoezi nje ya darasa ili kuendeleza ujifunzaji na kuwashirikisha wanafunzi katika shughuli za kijamii zinazokuza ujifunzaji • mazoezi yanayomhusisha mwanafunzi moja kwa moja • jinsi ya kuwashirikisha wazazi na walezi ili kuimarisha uwajibikaji. Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Kitabu cha Mwanafunzi kina Mwongozo wa Mwalimu ambao pia una mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwalimu atahitaji ili kumwongoza mwanafunzi aweze kufaulu katika mtalaa huu mpya wa Umilisi.

Authors

Language

Publisher

ISBN

9780195746839

Number Of Pages

0

File Size

13.10 mb

Format

EPUB

Edition

1

Published

01-01-2019